Amba
in Genre - Culture Genre - Imagination Genre - Reflection PH 2016 (Poems) Poems - Kiswahili Poems by Prof. Kithaka Wa Mberia

Amba/ MCHEZO WA KARATA

By Prof. Kithaka Wa Mberia

I will sing “AMBA”

So that I may

When I conclude, the saying

I will have explained

The crocodile’s behaviour

About his bragging

And those who fear to say

Anything in the farm

I proclaim saying

This crocodile

Is the rock

That defiles the farm

But then I say

Although he’s armoured himself

With a hard shell

He will rout not the rope

That crushes rocks

In the farm

We have seen crocodiles

Who bragged

They feared not the owners of the farm,

They routed not

The farmers’ rope

When the farmers started speaking

And tauted the rope tight

In the farm

If you see, an enunciator

Who values enunciation

I will retort,

I don’t seek void utterances,

But the crocodile

Who swaggers,

And the owners the farm

Frightened to talk

Cause me to speak

I will conclude, “SAYING”

Emphasising that

When the farm owners’ rope is stretched tout

As they start to speak,

That the witless crocodile

Will fail not to implore:

I was wrong to swagger

Declaring that

I, the crocodile

I’m already armoured

Sheathed in scales

To stifle the non sayers

In the farm

When they decide to speak

Nitaimba –“AMBA”

Hivi kwamba

Nimalizapo kwamba

Nitakuwa nimeamba

Juu ya mamba

Mwenye kujigamba

Na wacheleao kwamba

Katika shamba

Natangaza kwamba

Huyu mamba

Ndiye mwamba

Onaoharibu shamba

Bali namba

Ingawa amejipamba

Kwa magamba

Hatashinda kamba

Ivunjayo miamba   

Kwenye mashamba

Tumeshuhudia mamba

Ambao walijigamba

Kutoogopa wanashamba

Hawakushinda kamba

Ya wanashamba

Walipoanza kwamba

Na kuvuta kamba

Katika shamba

Ukiona muamba

Apendaye kwamba

Nitajibu kwamba

Sitafuti kwamba

Bali mamba

Mwenye kujigamba

Na wanashamba

Waogopao kwamba

Wamenifanya kuamba

Nitahimisha “-AMBA”

Nikikariri kwamba

Ivutwapo kamba

Ya wanashamba

Waanzapo kuamba

Jahili mamba

Hatakosa kuamba:

Nilikosea kujigamba

Nikiamba kwamba

Mimi mamba

Tayari nimejipamba

Kwa magamba

Kuzima wasioamba

Katika shamba

Waamuapo kuamba